1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Umoja wa Ulaya na Marekani hazikubaliani juu ya utoaji wa gesi ya Carbon

1 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5g

Umoja wa Ulaya na Marekani zimekubaliana kwamba Ongezeko la ujoto duniani ni suala muhimu linalopasa kupewa kipaumbele.

Katika mkutano wa siku moja baina ya wajumbe wa Umoja huo na Marekani mjini Washington rais Bush na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani pamoja na rais wa tume ya umoja wa Ulaya Jose Manuel Barrso walishindwa kufikia makubaliano juu ya utoaji wa gesi ya Carbon ijapokuwa rais Bush alisisitiza msimamo sawa.

Pande hizo mbili lakini ziliafikiana kuhusu kuweka huru safari za ndege na kupunguza vikwazo vya urasimu.

Rais Bush pia aliitolea mwito Urussi kushiriki katika mipango ya kuweka mfumo wa makombora ya ulinzi barani Ulaya akisema mipango hiyo inalenga kupambana na vitisho kutoka nchi kama Iran na sio kuichokoza Moscow.

Wajumbe katika mkutano huo walijadiliana pia kuhusu jinsi ya kuuzuia mpango wa Kinuklia wa Iran unaodaiwa ni wa kutengeneza silaha za Kinuklia.