1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Robert Mueller

Robert Swan Mueller III ni wakili wa Kimarekani na afisa wa serikali aliehudumu kama mkurugenzi wa sita wa shirika la upelelezi la Marekani FBI kuanzia 2001 hadi 2013. Alikuwa mchunguzi maalumu wa wizara ya sheria.

Mei 17, 2017 Robert Mueller aliteuliwa na naibu mwanasheria mkuu wa Marekani Rod Rosenstein kuwa mchunguzi maalumu kusimamia uchunguzi juu ya madai ya uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2016 na masuala yanayohusiana nao. Mueller alikabidhi ripoti yake kwa mwanasheria mkuu William Barr Machi 22, 2019. Aprili 18, 2019 wizara ya sheria ilitangaza ripoti ya mwisho ya uchugnuzi wa Mueller. Mei 29, 2019 Mueller alijiuzulu rasmi nafasi yake na ofisi yake ikafungwa. Katika ukurasa huu utapata maudhui za DW kuhusu Robert Mueller na kazi yake.

Onesha makala zaidi