1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Uchaguzi wa Marekani 2020

Wamarekani watamchagua rais wao mpya Novemba 3, 2020. Mgombea urais wa chama cha Democratic, Joe Biden, anapambana na rais wa sasa Donald Trump katika kinyang'anyiro kikali.

Donald Trump, rais wa 45 wa Marekani anataka kuchaguliwa tena kuwa rais kwa muhula wa pili kama mgombea wa chama cha Republican. Mpaka sasa marais 16 wa Marekani wameshinda mihula miwili mfululizo. Makamu wa rais wa zamani wa Marekani, Joe Biden, aliwapiku wagombea 29 kushinda uteuzi wa chama cha Democratic kama mgombea urais. Mnamo tarehe 11 Agosti, Biden alimteua mpinzani wake wa zamani katika chaguzi za awali, seneta wa jimbo la California, Kamala Harris, kuwa mgombea mwenza.

Onesha makala zaidi