1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Ursula von der Leyen

Ursula von der Leyen ni mwanasiasa wa Ujerumani ambaye amehudumu kama waziri wa ulinzi tangu 2013. Mwanachama huyo wa chama cha siasa za wastani za mrengo wa kulia - CDU, ndiyo mwaname wa kwanza kushika wadhifa huo.

Ursula von der Leyen, mzaliwa wa Brussels na mzungumzaji wa asili wa Kifaransa na Kijerumani, ni mtaalamu wa afya. Ni wazirii pekee aliehudumu katika baraza la mawaziri la Kansela Angela Merkel tangu alipochaguliwa kushika wadhifa huo mwaka 2005, kwanza kama waziri wa familia na vijana (2005-2009), kisha waziri wa ajira na masuala ya kijamii (2009 -2013) kabla ya kuwa waziri wa ulinzi 2013. Julai 02, 2019, viongozi wakuu wa mataifa ya Umoja wa Ulaya walimteuwa von der Leyen kuwa rais wa halmashauri kuu ya umoja huo, baada ya majadiliano makali yaliyofuatia uchaguzi wa bunge la Ulaya mwezi Mei, 2019. Ukurasa huu ni mkusanyiko wa maudhui zinazomhusu von der Leyen.

Onesha makala zaidi