1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron kuihamasisha tena Ulaya kuacha kuitegemea Marekani

Lilian Mtono
25 Aprili 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron hii leo anatarajiwa kuzungumzia maono yake ya kuwa na Ulaya yenye nguvu zaidi, na kuwashinikiza zaidi wanachama wa Umoja wa Ulaya kutoitegemea Marekani.

https://p.dw.com/p/4f9mu
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais Emmanuel Macron kuihamasisha kwa mara nyingine Ulaya kuacha kuitegemea Marekani katika kusuluhisha masuala yakePicha: Sebastien Nogier/AP/picture alliance

Rais Macron pia anatarajia kutumia fursa hiyo kuimarisha kampeni ya chama chake katika uchaguzi wa Ulaya.

Macron anarejea na masuala yaleyale aliyoitoa Septemba 2017 miezi kadhaa baada ya kuwa rais, lakini katika muktadha ambao katika kipindi cha miaka saba umekumbwa na changamoto kama za Brexit, janga la UVIKO-19 na uvamizi wa Urusi kwa Ukraine.

Macron anapigania dhana ya uhuru wa kimkakati ndani ya Ulaya katika sekta za uchumi na ulinzi, akisema wanahitaji kukabiliana na mizozo kama uvamizi wa Urusi nchini Ukraine bila kutegemea Marekani.

Anatoa hotuba hiyo wakati Umoja wa Ulaya ukiandaa ajenda yake mpya ya kimkakati ya kati ya mwaka 2024-2029.