1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Emmanuel Macron

Emmanuel Macron ni mwanasiasa wa nchini Ufaransa, mtumishi wa umma na mkurugenzi wa zamani wa benki ya uwekezaji. Alizaliwa Desemba 1977 mjini Amiens kaskazini mwa Ufaransa kwa wazazi - Daktari na profesa wa nyurolojia.

Harakati za Macron kuwania urais zilianza 2016 alipojienguwa kwenye chama cha rais Msoshalisti Francois Hollande na kuanzisha vuguvugu lake huru la En Marche! (Songa Mbele). Aliwasajili maelfu ya watu wa kujitolea waliokwenda nyumba kwa nyumba wakati wa kiangazi kusikiliza mawazo na maoni ya raia na En Marche! imejizolea uungwaji mkono mkubwa sana. Kulingana na mtandao wake, watu 200,000 wamejiunga na vuguvugu hilo chini ya mwaka mmoja. Ikiwa chunguzi za maoni za sasa ni jambo la kuaminika basi Macron ndiye rais ajaye wa Ufaransa.

Onesha makala zaidi