1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa EU kujadili kuhusu ulinzi wa anga wa Ukraine

22 Aprili 2024

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana leo hii nchini Luxembourg kujadili namna ya kuimarisha ulinzi wa anga wa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4f287
Ufaransa IViongozi wa Ulaya katika Mkutano wa kilele mjini Paris
Kuanzia kulia: Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Stephane Séjourné, wa Ujerumani Annalenna Baerbock na Janez Lenarcic, Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na Misaada ya KibinadamuPicha: Thomas Koehler/IMAGO

 Hayo yanajiri katika wakati ambapo Urusi imekuwa ikizidisha mashambulizi ya anga na kuilenga miundombinu ya nishati ya Ukraine.

Kyiv na washirika wake walipata msukumo baada ya Baraza la Wawakilishi la Marekani kuidhinisha mwishoni mwa juma kifurushi cha dola bilioni 60 kwa Ukraine ili kukabiliana na uchokozi wa Urusi.

Soma pia: Zelensky ataka NATO kujadili ulinzi wa anga wa Ukraine

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg wamekuwa wakizitaka nchi za Ulaya kuongeza juhudi zao katika kuipatia silaha Ukraine, hasa mifumo ya ulinzi wa anga.

Mawaziri hao wanatazamiwa pia kujadili vita vinavyoendelea nchini Sudan na Mashariki ya Kati ambapo wanalenga kutanua vikwazo zaidi dhidi ya Iran.