1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Haki za binadamuAfrika Kusini

Mahakama ya Haki barani Ulaya kutathmini rufaa ya Semenya

Saleh Mwanamilongo
23 Aprili 2024

Mahakama ya Haki barani Ulaya - ECHR imethibitisha kuwa itatathmini rufaa iliyowasilishwa na bingwa mara mbili wa Olimpiki Caster Semenya.

https://p.dw.com/p/4f6f2
Mwariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya
Mwariadha wa Afrika Kusini Caster SemenyaPicha: Christine Olsson/TT/IMAGO

Mwanariadha huyo wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 33 alishinda kesi iliyodumu kwa muda mrefu mnamo Julai mwaka jana dhidi ya Uswisi katika mahakama ya haki ya Ulaya.

Mahakama hiyo ilitoa uamuzi kuwa yeye ni mwathirika wa ubaguzi kutoka kwa Mahakama ya Usuluhishi wa migogoro Michezoni yenye makao makuu yake mjini Lausanne, Uswisi.

Lakini maafisa wa Uswisi, wakiungwa mkono na chama cha riadha ulimwenguni, wamelipeleka suala hilo katika jopo kuu la Mahakama ya ECHR, ambayo maamuzi yake lazima yatekelezeke, huku vikao vya kusikilizwa kwa kesi hiyo vikipangwa kuanza Mei 15.