1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Nasema Sitaki!

Udhalilishaji wa kingono dhidi ya watoto ni tatizo ambalo linaongezeka siku hadi siku duniani kote likiwa na athari kubwa kwa afya ya watoto, utu wao na fursa walizonazo katika maisha.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto, UNICEF, limekadiria wasichana zaidi ya milioni 120 ulimwenguni kote chini ya umri wa miaka 20 wamekabiliwa na ngono ya lazima au matendo mengine ya ngono ya kulazimishwa. Wasichana huripoti matukio ya unyanyasaji wa ngono angalau mara tatu zaidi kuliko jinsi wavulana wanavyoripoti, ingawa wavulana nao pia wako hatarini. Kupitia kampeini kwa jina "Nasema Sitaki" Idhaa ya Kiswahili ya DW inakuletea mfululizo wa ripoti, makala na video mwezi mzima wa Machi 2019 kuhusu visa na matukio ya udhalilishaji wa kingono kwa watoto.