Nusu-finali Kombe la Ulaya
24 Juni 2008Baada ya mapumziko ya siku 2, kombe la Ulaya la mataifa linarudi uwanjani jumatano hii kwa nusu finali ya kwanza-Ujerumani ikicheza na Uturuki,mjini Basel,Uswisi.
Kesho itakua zamu ya Spian iliovunja mwiko wa miaka 88 wa kutowafunga mabingwa wa dunia-Itali kukata tiketi yao ya finali wakitoana jasho na Urusi.Urusi iliipiga kumbo Holland baada ya kurefushwa mchezo.Ni timu gani 2 zitacheza finali ya kombe hili jumapili ijayo ndilo swali analouliza kila mmoja na si rahisi kulijibu kwa jicho la maajabu mengi yaliotokea tangu kuanza kombe hili la Ulaya:
Tukianza na changamoto ya kesho kati ya spain na Russia, ni wazi waspain wamebidi kusahau mpambano wao wa awali na Urusi walipoikomea mabao 4:1 na wanajua wazi kesho itakua timu tofauti sana ile walioichezesha kindumbwendumbwe.Baada ya kuilaza holland chini ya kocha wao mdfachi Guus Hiddink,amepanga mtego mwengine kesho wa kuweana
►◄