1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

NSA

Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani ni shirika la ujasusi la serikali ya Marekani, lenye dhima ya kufuatilia mambo ya kimataifa, kukusanya na kuchambua taarifa za ujasusi wa kimataifa.

NSA pia ina jukumu la kulinda mawasiliano ya Marekani na mifumo ya mawasiliano isiingiliwe na dhidi ya vita vya mtandaoni. Uchunguzi wa NSA umekuwa ukizusha mizozo ya mara kwa mara, mfano udukuzi wake wa viongozi waliokuwa wanapinga vita vya Vietnam au udukuzi wa kiuchumi. Mwaka 2013 ukubwa wa programu za udukuzi za NSA ulifichuliwa kwa umma na Edward Snowden. Kulingana na nyaraka zilizofichuliwa, NSA inadukuwa mawasiliano ya watu zaidi ya bilioni moja duniani, wengi wao wakiwa raia wa Marekani na hata wahsirika wakuu wa Marekani katika mataifa ya kigeni.

Onesha makala zaidi