MUNICH: Robert Gates amekanusha shutuma za Vladimir Putin
11 Februari 2007Matangazo
Waziri wa ulinzi wa Marekani,Robert Gates amekanusha shutuma za Rais Vladimir Putin wa Urussi kwamba Washington imesababisha mataifa kuwania kutengeneza silaha.Gates alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa usalama wa kimataifa mjini Munich,kusini mwa Ujerumani. Wakati huo huo alisema,wanachama wa Shirika la Kujihami la nchi za Magharibi-NATO-wanapaswa kushirikiana na Urussi katika masuala ya usalama. Waziri Gates ametoa hotuba hiyo,siku moja baada ya Putin kuuambia mkutano huo kuwa matumizi ya nguvu za kijeshi ya Marekani,yanachochea mataifa madogo kuanzisha miradi ya silaha za nyuklia.