1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Bobi Wine

Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kwa jina la kisanii Bobi Wine, ni mwanasiasa, mfanyabiashara, mhisani, mwanamuziki na muigizaji nchini Uganda. Amekuwa mbunge wa Kyadondo Masahriki tangu Julai 11, 2017.

Bobi Wine alizaliwa Februari 12, 1982 katika hospitali ya Nkozi ambako marehemu mama yake alikuwa akifanya kazi. Wanachama wa familia yake wana asili yao katika iliyokuwa wilaya ya Mpigi, ambayo kwa sasa ni wilaya ya Gomba. Alikulia katika eneo la mabanda la Kamwokya, kaskazini-mashariki mwa Kampala, mji mkuu wa Uganda. Mwaka 2017, Bobi Wine alitangaza kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kyadondo Mashariki na kuendesha kampeni ya nyumba hadi nyumba iliyowavutia watu wengi. Alishinda uchaguzi huo kwa tofauti kubwa sana ya kura dhidi ya mgombea wa chama tawala cha NRM na pia mgombea wa chama kikuu cha upinzani cha FDC. Mwaka 2018, Bobi Wine alizidi umaarufu, na kuongoza ushindi katika chaguzi kadhaa ndogo kwa wagombea aliowapigia kampeni, na hivyo kuwachachafya wagombea wa chama tawala pamoja na wale wa FDC. Ukurasa huu ni mkusanyiko wa maudhui za DW kuhusu Bobi Wine.

Onesha makala zaidi