1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Bobi Wine

Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kama Bobi Wine ni mwanasiasa, mfanyabiashara, na msanii kutoka nchini Uganda. Kuanzia Julai 11, 2017 anawakilisha jimbo la Kyadondo Mashariki katika bunge la taifa la Uganda.

Bobi alizaliwa Februari 12, 1982 katika iliyokuwa sehemu ya wilaya ya Mpigi ambayo sasa ni wilaya ya Gomba. Alikulia katika eneo la mabanda la Kamwookya, kaskazini-mashariki mwa mji mkuu waUganda Kampala. Alisomea muziki katika chuo kikuu cha Makerere. Februari 2018, alijiunga na kozi ya uongozi wa karne ya 21 katika shule ya masomo ya kiserikali ya John F. Kennedy sambamba na viongozi kutoka mataifa mengine.

Onesha makala zaidi