1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Human Rights Watch

Human Rights Watch ni shirika lisilo la kiserikali la kimataifa, linalofanya utafiti na uraghibishi juu ya haki za binaadamu.

Makao makuu ya Human Rights Watch yako mjini New York, Marekani na pia lina ofisi katika miji ya Amsterdam, Beirut, Berlin, Brussels, Chicago, Geneva, Johannesburg, London, Los Angeles, Moscow, Nairobi, Paris, San Francisco, Sydney, Tokyo, Toronto, Washington DC na Zurich. HRW ilianzishwa mwaka 1978 kama shirika lisilo la kiserikali nchini Marekani, kwa jina la Helsinki Watch, kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya Helsinki na Muungano wa zamani wa Kisovieti. Baadae lilikuja kubadilishwa jina baada ya kutanuwa shughuli zake kujumlisha maeneo mengi zaidi ya dunia.

Onesha makala zaidi