1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Wakfu wa Bill na Melinda Gates

Wakfu wa Bill na Melinda Gates ndiyo wakfu binafsi mkubwa zaidi duniani unaoendeshwa kwa uwazi zaidi. Wakfu huo ulianzishwa na Bill na Melinda Gates mwaka 2000.

Malengo makuu ya wakfu huo ni kuboresha huduma za afya na kupunguza umaskini duniani, na nchini Marekani, kupanua fursa za elimu na upatikanaji wa teknolojia za mawasiliano. Wakfu huo wenye makao yake mjini Seatle Washington, unadhibitiwa na wadhamini wake wakuu watatu – Bill Gates, Melinda Gates na Warren Buffet. Kufikia Desemba 2014, wakfu huo ulikuwa na mtaji wa dola za Marekani bilioni 44.3. Katika ukurasa ufuatao, utapata mkusanyiko na maudhui za DW kuhusu Wakfu wa Bill na Melinda Gates na viongozi wake wakuu.