LUXEMBOURG: Nchi za Ulaya zisaidiane mzigo wa wakimbizi | Habari za Ulimwengu | DW | 12.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LUXEMBOURG: Nchi za Ulaya zisaidiane mzigo wa wakimbizi

Malta imetoa mwito kwa nchi za Umoja wa Ulaya kusaidia kuwapokea wakimbizi na waomba hifadhi ya kisiasa.Mwito huo umetolewa kabla ya kufanywa mkutano wa mawaziri wa nje wa Umoja wa Ulaya kujadili njia za kurekebisha sheria kuhusika na wakimbizi na waomba hifadhi ya kisiasa.Kila mwaka Waasia na Waafrika kwa maelfu,wanavuka Bahari ya Mediterania wakijaribu kukimbilia nchi za Umoja wa Ulaya kwa kupitia Malta,Italia na Hispania. Mkutano wa mawaziri wa ndani wa Umoja wa Ulaya umeitishwa baada ya Malta kulaumiwa kwa kukataa kuwachukua watu 27 waliokuwa wakingangania nyavu za uvuvi kwa siku tatu,huku Malta na Libya zikibishana nani awaokoe.Malta na Hispania zinaamini,wakimbizi wanaopatikana baharini katika maeneo ya kimataifa,wasambazwe nchi za Umoja wa Ulaya - na nchi zilizo kubwa ndio zibebe sehemu kubwa ya mzigo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com