1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Wakimbizi

Kulingana na mkataba wa Geneva kuhusu wakimbizi, mkimbizi ni mtu alie nje ya chi yake ya uraia kwa sababu wana misingi sahihi ya kuwa na hofu ya kuteswa na hawawezi kupata hifadhi ndani ya nchi yake.

Katika mukhtadha wa Umoja wa Mataifa, tafisri wa ukimbizi imepanuliwa na kujumlisha vizazi vya wakimbizi kwa makundi mawili: Wakimbizi wa Kipalestina na Wasahrawi. Kwa sasa Umoja wa Mataifa hautambui ukimbizi wa kurithi nje ya makundi hayo mawili. Kufikia katikati mwa 2015, kulikuwepo na wakimbizi milioni 15.1 wanaohudumiwa na shirika wakimbizi la kimataifa UNHCR - idadi ambayo ndiyo kubwa zaidi katika kipindi cha miaka 20. Wakimbizi wengine milioni 5.1 wanahudumiwa katika kambi karibu 60 katika eneo la Mashariki ya Kati. Ukurasa huu unakukusanyia maudhui za karibuni za DW kuhusu wakimbizi.

Onesha makala zaidi