1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaDjibouti

Watu 21 wamekufa baada ya boti ya wahamiaji kuzama Djibouti

24 Aprili 2024

Idadi ya watu waliokufa imefikia 21 huku wengine 23 wakiwa hawajulikani waliko, baada ya kutokea ajali ya boti ya wahamiaji katika pwani ya Djibouti.

https://p.dw.com/p/4f75F
Ajali ya boti Djibouti
Miili ya watu waliokufa katika ajali ya boti karibu na pwani ya mji wa Obock:09.04.2024Picha: International Organization for Migration/AP/picture alliance

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji - IOM limesema boti iliyokuwa na wahamiaji 77 wakiwemo watoto, ilizama katika pwani ya taifa hilo.

Msemaji wa IOM Yvonne Ndege amesema wanashirikiana na maafisa wa Djibouti  katika juhudi za uokoaji.

Aprili 8, Boti nyingine iliyokuwa na zaidi ya watu 60 ilizama katika pwani ya Godoria.  Takriban wiki mbili zilizopita, boti nyingine iliyowabeba wahamiaji, wengi wao wakiwa raia wa Waethiopia ilizama katika pwani ya Djibouti na kusababisha vifo vya watu kadhaa.