1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

UNHCR yazindua hazina ya wahanga wa majanga ya hali ya hewa

24 Aprili 2024

Umoja wa Mataifa utazindua mfuko mpya wa kuchangisha fedha za kusimamia mpango wa kukabiliana na athari ya hali ya hewa inayolenga kuimarisha ulinzi kwa wakimbizi na jamii zilizohamishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

https://p.dw.com/p/4f9A1
UNHCR
Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi la UNHCR Filippo GrandiPicha: Jean-Guy Python/AFP-Pool/KEYSTONE/dpa/picture alliance

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limesema linalenga kuchangisha dola milioni 100 kwa ajili ya mfuko huo mpya ifikapo mwisho wa mwaka ujao kusaidia wakimbizi, jumuiya zinazowahifadhi na nchi zilizoathirika zaidi.

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi la UNHCR Filippo Grandi amesema athari za mabadiliko ya hali ya hewa zinazidi kuwa mbaya, zikizidisha migogoro, kuharibu maisha na, kusababisha watu kuyahama makazi yao.

UNHCR: Wakazi wa Gaza hawapaswi kuvuka kuingia Misri

Mfuko huo unalenga kuongeza upatikanaji wa rasilimali endelevu katika kambi za wakimbizi na mazingira mengine ya uhamisho. Ikiwa ni pamoja na kujumuisha upatikanaji wa nishati ya umeme, shule na miundombinu ya afya.