1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Nani anawaunga mkono majenerali wanaopigana Sudan?

16 Aprili 2024

Mzozo uliozuka nchini Sudan mwaka mmoja uliopita umeleta maafa makubwa katika maeneo mengi nchini humo, umesababisha janga la njaa kwa mamilioni ya watu, na kuleta mgogoro wa kibinadamu.

https://p.dw.com/p/4eqzT
Sudan | Mzozo |  Majenerali wa Sudan  Abdel Fattah Abdelrahman al-Burhan na Mohamed Hamdan Dagalo.
Majenerali wa Sudan Abdel Fattah Abdelrahman al-Burhan na Mohamed Hamdan DagaloPicha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Kumekuwa na mashaka ya kuwepo kwa ushawishi wa wahusika wa nje tangu kupinduliwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Omar al-Bashir miaka mitano iliyopita,baada ya kuzuka vuguvugu la kuupinga utawala wake. Lakini swali ni je? ni nani anayewaunga mkono majenerali wawili wanaokinzana nchini Sudan.

Mzozo unapoendelea kutokota nchini Sudan, Mahasimu wawili wa kijeshi wametafuta uungwaji mkono kutoka kwa wafadhili wa kigeni wakati kila upande unajaribu kuvutia upande wake.

Msaada huo unahatarisha kuongezeka, na kurefusha vita kati ya wanajeshi wa Sudan wakiongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na Kikosi cha wanamgambo cha (RSF) kinachoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kama Hemedti.

Ushawishi huu wa wafadhili wa kigeni umekuwa kigezo kikubwa nchini Sudan tangu kupinduliwa kwa serikali ya kiraia katika mapinduzi ya Oktoba 2021, hatua ambayo ilizuia kupatikana mabadiliko ya utawala baada ya ule wa kiimla uliokuwa ukiongozwa na Rais Omar al-Bashir, ambaye aliondolewa kwa nguvu madarakani.

Soma pia:Euro bilioni mbili zapatikana kwa ajili ya kuisaidia Sudan

Uaongozi wa  kipindi cha mpito uliojumuisha  vyama vya kiraia na ambao ukiungwa mkono na Jumuiya ya  kimataifa, uliwataka wanamgambo wa kundi la RSF kuachia madaraka lakini masuala mawili yalionesha kuwa bado yanazusha utata.

Suala la kwanza linahusu  hoja iliyotolewa na RSF ya kutaka  kikosi hicho kujumuishwa katika ratiba ya kawaida ya jeshi la taifa. Suala la  pili linahusu mamlaka ya uongozi  wa jeshi na mpangilio mzima wa madaraka ya usimamizi wa shughuli za kijeshi na suala la uangalizi wa kiraia.

Ushawishi wa kibiashara ni sehemu ya kuchochea mzozo?

Pande zote mbili pia zimekuwa zikishindana kuwania ushawishi wa kibiashara katika maeneo mbali mbali ya ndani ya nchi hadi  nje ya mipaka ya Sudan.

Mshirika wa wazi zaidi wa jenerali Al- Burhan ni Misri, inayopakana na Sudan ambapo zaidi ya watu 500,000 wamevuka tangu mapigano kuanza.

Tangu vita kuanza, Misri imemkaribisha jenerali huyo na wajumbe mara kadhaa,alipofanya ziara nchini humo.Misri pia ilianzisha mchakato wa amani unaohusisha majirani wa Sudan ambao ulienda sambamba na juhudi za upatanishi zinazoongozwa na Marekani,

Saudi Arabia na jumuiya ya ushirikiano wa maendeleo ya nchi za Mashariki na upembe wa Afrika, IGAD.

Eritrea, ni nchi nyingine jirani ambayo jenerali al Burhan amekuwa akitafuta uungwaji mkono kikanda na hasa baada ya kuonekana kuwa ni moja ya vituo vyake vya kwanza wakati alipoanza tena safari zake za nje ya Sudan  mwaka jana.

Soma pia:Mataifa ya Ulaya yafanya kongamano kuichangia fedha Sudan

Vyanzo vinasema kuwa tangu mwishoni mwa 2023, jeshi pia limepata msaada wa mali kutoka Iran, ikiwemo droni zilizotengenezwa na Iran ambazo ziliisaidia kupata mafanikio makubwa katika harakati zake katika uwanja wa vita huko Omdurman,mji ambao ni sehemu ya mji mkuu Khartoum.

Kwa upande wake RSF kikosi kinachoongozwa na Hemedti, kwa miaka kadhaa, mshirika muhimu zaidi wao amekuwa Umoja wa Falme za Kiarabu.

Wachambuzi waangalia ushawishi wa kikanda

Vyanzo vya Sudan, wachambuzi na wanadiplomasia wanasema Umoja wa Falme za Kiarabu umejaribu sana kurejesha ushawishi wa Kiislamu

katika eneo hilo, kwa kuingilia kati migogoro ya ndani ya nchi kadhaa za eneo hilo zikiwemo Libya na Yemen.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifawanasema taarifa zinazoonesha kwamba Umoja wa Falme za Kiarabu, imetuma silaha kwa RSF kupitia mashariki mwa Chad ni "za kuaminika", na kwamba  vyanzo hivyo katika nchi za Chad na Darfur viliripoti kuwa ndege za mizigo ziliwasilisha silaha hizo na risasi mara kadhaa kwa wiki.

Mwaka mmoja wa vita vya Sudan

Umoja wa Falme za Kiarabu umekanusha madai ya kusafirisha bidhaa kama hizo ikieleza kwamba jukumu lake nchini Sudan linalenga kutowa msaada wa kibinadamu na wito wa kusitishwa kwa mapigano.

Ripoti iliyochapishwa Januari mwaka huu na Umoja wa Mataifa imesema kuwa RSF, ambayo imekuza miungano ya kikabila inayoenea kote kwenye

Soma pia:Marekani kuhimiza ufadhili zaidi wa jumuiya ya kimataifa kwa mzozo wa Sudan

mipaka ya magharibi ya Sudan, ilileta silaha nchini Sudan kutoka Libya na Jamhuri ya Afrika ya Kati, mafuta kutoka Sudan Kusini, na kuimarisha  mahusiano pamoja na Urusi.

Nchi zenye nguvu katika kanda ya Afrika Mashariki,Ethiopia na Kenya nazo zinaushawishi kwa kiasi fulani kutokana na jukumu lao katika juhudi za kidiplomasia kwenye eneo hilo na katika juhudi zilizotangulia za  upatanishi katika mgogoro wa Sudan.