LONDON: al Bashir ashutumu nchi za magharibi | Habari za Ulimwengu | DW | 01.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: al Bashir ashutumu nchi za magharibi

Rais Omar al Bashir wa Sudan amezilaumu nchi za magharibi kwa matatizo ya nchi yake na hasa katika jimbo la Darfur.

Akizungumza katika mahojiano na gazeti la Guardian la Uingereza rais al Bashir amezilaumu Marekani, Ufaransa na Uingereza kwa kuyahujumu mazungumzo juu ya kuutatua mgogoro wa Darfur.

Rais huyo ameitaka hasa serikali ya Uingereza iombe radhi kwa sababu ya kuitolea Sudan vitisho vya vikwazo ikiwa mazungumzo hayo yatashindikana.

Kiongozi huyo wa Sudan pia amezishutumu nchi hizo kwa kuendesha siasa ya kuidhinisha vikwazo katika ngazi ya kimataifa ili kuiadhibu nchi yake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com