1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Palestina

Wapalestina wapatao milioni 10 au 11 wamegawika katika makundi mawili – Wapalestina wa Kihistoria na wale walioko ngambo, hasa katika mataifa jirani ya Kiarabu.

Juhudi za kuunda taifa la Kipalestina katika kingo za magharibi mwa Mto Jordan zimekwamishwa na migogoro ya mara kwa mara na Israel, pamoja na mvutuano juu ya hadhi ya Wapalestina walioko ngambo. Vita vilivyofuatia kutangazwa kwa uhuru wa Israel mwaka 1948 vilisababisha kugawanywa kwa koloni la zamani la Uingereza la Palestina, kati ya Israel, Jordan na Misri. Mamia kwa maelfu ya Wapalestina walitoroka au kufukuzwa kwenye maeneo yao ya asili wakati wa vita hivyo, katika kile wanachokiita “Nakba” au Janga.

Onesha makala zaidi