1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel inaweza kulitokomeza kabisa kundi la Hamas?

12 Desemba 2023

Kuangamizwa kabisa kwa kundi la wanamgambo wa Hamas ni moja ya malengo yaliyotajwa kwenye kampeni kubwa ya kijeshi ya Israeli katika Ukanda wa Gaza. Lakini swali ni je, Israel inaweza kulitokomeza kundi hilo?

https://p.dw.com/p/4a4bl
Ukanda wa Gaza | Moshi ukifuka angani baada ya mashambulizi ya Israel
Moshi ukifuka angani baada ya mashambulizi ya vikosi vya Israel eneo la Ukanda wa GazaPicha: Clodagh Kilcoyne/REUTERS

Mashambulizi ya anga na ardhini, yaliyochochewa na shambulio la kushtukiza la kundi la Hamas dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7, yameenea hadi kusini mwa Gaza.

Mapigano bado yanaendelea kaskazini mwa ukanda huo, ingawa Israel inasemaHamas ilipoteza udhibitikatika eneo hilo mwezi mmoja uliopita.

Mike Martin, afisa wa zamani wa jeshi la Uingereza na mtafiti mwandamizi katika idara ya mafunzo ya vita katika chuo kikuu cha Kings mjini London, amesema mikakati ya sasa ya Israel huenda ikalidhoofisha kundi la Hamas lakini haitafikia lengo la kuliangamiza kundi hilo.

Martin ameongeza kuwa kile ambacho Israel inatafuta kwasasa ni chaguo pana la matumizi ya pamoja ya silaha yanayojumuisha makombora, ndege zisizo na rubani pamoja na mizinga.

Israel inaweza kuharibu mahandaki, baadhi ya hifadhi za silaha na baadhi ya viongozi, lakini je itaweza kumuua kila mwanamgambo wa Hamas kwa sasa? Hapana, haitaweza," Alisema Martin

Soma pia:Israel: Mashambulizi yatasitishwa tutapoitokomeza Hamas

Aliongeza kwamba jeshi la Israel huenda lisifanikiwe kwa kiwango kikubwa katika kulitokomeza kundi la Hamas kwa sababu idadi yao ni maelfu na wote wamechanganyika na raia wa kawaida.

Katika muktadha huu, Martin anasema kuwa ahadi ya Israel ya kupunguza vifo vya raia ni jambo lisilowezekana kabisa.

Akisisitiza kuwa kufanya kampeini hii kubwa ya kijeshidhidi ya adui asiye wa kawaida aliyejificha katika maeneo ya mijini yenye raia wengi haiwezekani, hali ambayo baadaye inaunda kizazi kijacho cha wanamgambo ambao watakuwa wakipigana katika muda wa miaka mitano au kumi ijayo.

Hamas ni vuguvugu lililo hai katika Ukanda wa Gaza

Kile ambacho Israel inaonekana  kufanya ni kuondoa uwezekano wa mtu yeyote kuitawala Gaza lakini sio lazima kundi la Hamas ambalo ni nguvu hai katika ukanda huo wa Gaza na jamii.

Ukanda wa Gaza | Wanajeshi wa Israel wakiwa katika mawindo kushambulia Hamas
Wanajeshi wa Israel wakiwa katika eneo la vita katika Ukanda wa GazaPicha: Ohad Zwigenberg/AP Photo/picture alliance

Nathan Brown, profesa na mwanasayansi katika chuo kikuu cha George Washington, maalumu kwa siasa za Palestina, anasema vita hivyo na hasara iliyosababisha,vinaongeza umaarufu wa Hamasmiongoni mwa baadhi ya Wapalestina.

Brown ameongeza kuwa kwa kiasi fulani, Hamas inaibuka kuwa na nguvu zaidi kisiasa katika maeneo mengine ya jamii ya Wapalestina.

"Tangu wakati huo [Oct 7], mashambulizi ya Waisraeli ni ya nguvu mno na uongozi wa Palestina ni dhaifu sana, kimsingi hakuna umuhimu." Alisema 

Aliongeza kwamba "kwa hivyo kwasasa, kama wewe ni Mpalestina, unaona, sawa, watu pekee ambao wanachukuwa hatua kwa ajili yetu ni Hamas."

Huku Israel ikisema inalenga kuuangamiza uongozi wa juu wa Hamas, Brown anaona kwamba hilo halitazuia kundi hilo kuwepo.

Wataalamu wanasema suluhisho la kisiasa linakosekana kwa sasa ambalo ni muhimu katika kutokomeza Hamas au vitisho vya usalama kutoka makundi yoyote yatakayofuata.

Soma pia:Israel yakanusha kutaka kuwahamishia Misri wakaazi wa Gaza

Maelfu ya Wapalestina wameuawa tangu vita kuanza huku wengi miongoni mwa idadi ya watu milioni 2.3 katika ukanda wa Gaza wametoroka makazi yao na wanakosa chakula, maji na huduma za matibabu.

Wataalamu wa magonjwa ya akili katika eneo hilo, wanasema watoto wengi wanaonyesha dalili za kiwewe.

Kundi la Hamas linachukuliwa na Israel, Umoja wa Ulaya, Ujerumani ikiwepo na Marekani kuwa kundi la wanamgambo. Kundi hilo lilishinda uchaguzi wa ubunge wa Palestina mwaka 2006 na kuchukuwa udhibiti wa ukanda wa Gaza mnamo mwaka 2007.

Vikosi vya Israel vyaonesha silaha zilizofichwa katika mdoli