1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Morocco

Falme ya Morocco ndiyo ilioko magharibi zaidi miongoni mwa nchi za Kiarabu -- ikijulikana pia kama "Maghreb". Inapakana na bahari za Atlantiki na Mediterrania, na ina historia ya uhuru isiyofanana na ya jirani zake.

Utamaduni wa Morocco ni mchanganyiko wa tamaduni za Kiarabu, Berber, Ulaya na Afrika. Morocco ilikuwa nchi lindwa ya Ufaransa kuanzia 1912 hadi 1956 wakati Sultan Mohammed alipokalia kiti cha ufalme. Alirithiwa na mwanae wa kiume Hassan II alietawala kwa miaka 38 na kutoa mchango mkubwa katika juhudi za kusaka amani ya Mashariki ya Kati. Lakini pia alidandamiza vibaya upinzani wa ndani. Mwanae Mohammed VI alirithi kiti hicho cha ufalme mwaka 1999. Morocco ilirejeshewa kiti chake katika Umoja wa Afrika mwaka wa 2017 baada ya kujiweka nje kwa zaidi ya miaka 30 kuhusiana na suala la Sahara Magharibi.

Onesha makala zaidi