1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Al-Shabaab

Al-Shabaab (vijana) ni kundi la wapiganaji wa siasa kali lenye makao yake Somalia. Kundi hili lilianzishwa kati ya 2004 na 2006 likidai linapigania kuanzishwa kwa utawala wa Kiislamu kwenye Pembe ya Afrika.

Al-Shabaab linadhibiti maeneo makubwa ya kusini na kati ya Somalia, na lina mafungamano na makundi mengine ya kigaidi kama vile al-Qaida na Boko Haram. Wapiganaji wake wamefanya mashambulizi kwenye maeneo kadhaa ya Pembe ya Afrika, yakiwemo yale ya mwaka 2013 kwenye jengo la maduka mengi la Westgate jijini Nairobi, Kenya, ambayo yalipoteza maisha ya zaidi ya watu 60.

Onesha makala zaidi