1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Al Qaeda

Kundi hilo la kigaidi lililohodhi sehemu kubwa ya miongo miwili, Al Qaeda imepoteza udhibiti wake kwa makundi kama vile "Dola la Kiislamu." Licha ya kuuawa kwa kiongozi wake Osama bin Laden 2011, kundi hilo linaendelea.

Likiwa limeundwa mwaka 1988 na kuongozwa na Osama bin Laden kuanzia 1989 hadi kifo chake mwaka 2011, kundi la al Qaeda liliendesha mashambulizi makubwa na ya ufanisi dhidi ya shabaha za Marekani na za kimataifa katika miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000. Shambulizi maarufu zaidi ni lile la Septemba 2001, ambapo ndege za abiria zilitumika kushambulia Jengo la Kituo cha Biashara Duniani WTO mjini New York na wizara ya Ulinzi ya Marekani mjini Washington, DC. Mwitikio kwa mashambulizi hayo hata hivyo uliliacha kundi la Al Qaeda katika maficho, la likiwa na maeneo machache ya kujificha baada ya muungano wa kijeshi ulioongozwa na Marekani kulifirusha katika maficho yake nchini Afghanistan. Huu hapa ni mkusanyiko wa maudhui za DW kuhusu Al Qaeda.

Onesha makala zaidi