1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Al-Nakba

Al-Nakba ni neno la Kipalestina linaloelezea matukio ya mwaka 1948, wakati Wapalestina wapatao 700,000 walipofukuzwa au kuyakimbia makaazi yao kufuatia kuundwa kwa taifa la Israel.

Siku ya Al-Nakba au Janga inaadhimishwa kila Mei 15, wakati Israel ikisherehekea kuundwa kwa taifa lake. Kwa Wapalestina ni siku ya maombolezi wakikumbuka matukio yaliotangulia na kufuatia tangazo la uhuru wa Israel mwaka 1948. Siku hii ilianzishwa na Yasser Arafat mwaka 1998.