1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina waadhimisha kumbukumbu ya miaka 76 ya Nakba

15 Mei 2024

Wapalestina wanafanya kumbukumbu ya miaka 76 leo tangu mamia kwa maelfu walipolazimishwa kuihama ardhi yao katika mapigano ambayo yaliyofungua njia ya kuundwa kwa taifa la Israel mnamo mwaka 1948.

https://p.dw.com/p/4fsEg
Wapalestina mwaka 1948
Wapalestina mwaka 1948Picha: ELDAN DAVID/EPA/dpa/picture-alliance

Wapalestina wanafanya kumbukumbu ya miaka 76 leo tangu mamia kwa maelfu walipolazimishwa kuihama ardhi yao katika mapigano ambayo yaliyofungua njia ya kuundwa kwa taifa la Israel mnamo mwaka 1948.

Inakadiriwa  zaidi ya Wapalestina 700,000 walikimbia au kuondolewa kwa lazima kutoka kwenye vijiji vyao na wengi walikwenda kutafuta hifadhi kwenye ardhi ambayo sasa ni Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi.

Kumbukumbu hiyo iitwayo Nakba, ambalo ni neno la Kiarabu linalomaanisha janga, inazingatiwa kuwa ndiyo chanzo cha masaibu yanayowakumba Wapalestina na chimbuko la mzozo wa Mashariki ya Kati.

Inafanyika katika wakati mamia kwa maelfu ya wakaazi wa Gaza wameukimbia mji wa kusini wa Rafah kuepuka operesheni ya ardhini inayotarajiwa kufanywa na vikosi vya jeshi Israel.

Mapema hapo jana Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alireja mwito wake wa kutaka yapatikane makubaliano ya kusitisha vita na kufunguliwa njia za kupelekwa misaada ya kiutu kwenye Ukanda wa Gaza.