Kansela Merkel asema mkutano wa Annapolis nafasi ya kupata amani
28 Novemba 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel alipohotubia bunge mjini Berlin aliyaeleza matokeo ya mkutano wa Annapolis kama ni nafasi ya kupata amani ya kudumu kati ya Israel na Wapalestina.
Wakati huo huo Merkel akasisitiza wajibu wa kihistoria wa Ujerumani kuhakikisha usalama wa Israel na kuwepo kwa taifa la Israel.