1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Angela Merkel

Angela Merkel ni mwanasiasa mashuhuri nchini Ujerumani, ndiye mwenyekiti wa chama cha Christian Democratic Union CDU, pia Kansela.

Merkel ndiye mwanamke wa kwanza kuwa Kansela wa Ujerumani na mmoja wa makansela waliohumu kwa muda mrefu, alichaguliwa kwa mara ya kwanza 2005 na ametokea kuwa kiongozi shupavu na anaeheshimika barani Ulaya na duniani kote. Aliongoza juhudi za kukabiliana na mgogoro wa fedha na wa madeni barani Ulaya. Msimamo wake usiyoyumba kuhusu suala la wakimbizi ulimjengea sifa duniani kote lakini pia ulikosolewa na wapinzania ndani na nje ya chama chake cha CDU. Jarida la Marekani la Time lilimtaja Merkel kuwa mtu maarufu zaidi kwa mwaka 2015.

Onesha makala zaidi