1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Miaka 30 baada ya kuporomoshwa kwa Ukuta wa Berlin

Tarehe tisa Novemba inatimia miaka 30 tangu kuanguka kwa ukuta wa Berlin. Ni siku muhimu sana katika historia ya Ujerumani inayokumbusha matukio ya mchanganyiko wa hisia za furaha na huzuni.

Kuanguka kwa ukuta wa Berlin ni tukio lililoibadilisha dunia. Miaka mitatu baadaye, Wajerumani waliungana baada ya kutenganishwa kwa muda wa miaka 41. Kutokana na kuangushwa kwa utawala wa pili wa kidikteta katika ardhi ya Ujerumani yaani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani, DDR, mfumo wote wa kisoshalisti barani Ulaya ulisambaratika. Vita baridi baina ya mashariki na magharibi vilizimika

Onesha makala zaidi