1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Iran

Iligeuka Jamhuri ya Kiislamu mwaka 1979, baada ya kuangushwa kwa utawala wa Kifalme na wahadhiri kuchukuwa udhibiti wa kisiasa chini ya kiongozi mkuu Ayatollah Khomeini.

Mapinduzi ya Iran yalitamatisha utawala wa Shah, ambaye aliyatenga makundi yenye nguvu ya kidini, na kisiasa kupita programu ya kuleta usasa na kuielekeza zaidi nchi upande wa Magharibi – programu ambayo iliambatana na ukandamizaji mkubwa zaidi wa wapinzani. Persia, kama Iran ilivyokuwa ikijulikana kabla ya 1935, ilikuwa moja ya himaya zenye nguvu zaidi za dunia ya kale, na kwa muda mrefu nchi hiyo imeendeleza utambulisho wake wa kitamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu, kwa kubakiza lugha yake yenyewe, na kufuata tafsiri ya Uislamu wa madhehebu ya Shia.

Onesha makala zaidi