1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je Syria ndio sababu ya Iran na Israel kushambuliana?

Angela Mdungu
24 Aprili 2024

Israel imekuwa ikiishambulia Syria kwa siri kwa muda mrefu, ikijaribu kuvishambulia vikosi vinavyoipinga ili kuvizuia visiwe na nguvu na wataalamu wana hofu kuwa mzozo wa Gaza, huenda ukafanya mambo kuwa mabaya zaidi.

https://p.dw.com/p/4f9FP
Bendera za madola ya Iran na Israel Picha: H. Tschanz-Hofmann/IMAGO

Wiki moja baada ya shambulio linalodaiwa kufanywa na Israel katika ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus April mosi,  Rais  wa Syria Bashar Al Assad aliendelea na shughuli zake kama ilivyo ada. Alijitokeza hadharani mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Iwapo alionekana kutokerwa na ukweli kwamba taifa la kigeni liliwaua majenerali kadhaa wangazi ya juu katika mji mkuu siku kadhaa tu zilizopita, basi hiyo ilikuwa ni makusudi, anasema Haid Haid, mchambuzi wa masuala ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka mjini London.


"Kuonekana kwake hakukuwa suala la bahati mbaya. Ilikuwa sehemu ya kampeni ya vyombo vya habari ili kutoa ujumbe kwa kila mtu kuwa kila kitu kinaendelea kama kawaida. Tulishuhudia Assad na mkewe wakishiriki Iftar mjini Tartous. Tuliwaona pia wakisherehekea Eid al-Fitr na watoto wake na mkewe mjini Damascus, nafikiri hii inaonesha ujumbe wake ulikuwa na sehemu mbili. Moja ni kuwa Syria haitoshiriki kuwa sehemu ya Iran katika kujibu mashambulizi ya Israel  bydhidi ya ubalozi mdogo wa Iran. Na pili ni kuwa Syria haitokuwa sehemu ya jukwaa au jukwaa lenyewe kwa ajili ya majibu hayo." Anasema mchambuzi Haid

Iran
Iran imeendelea kusema kuwa itajibu mashambulizi yoyote dhidi yake kutoka kwa adui yake IsraelPicha: Morteza Nikoubazl/NurPhoto/picture alliance

Israel yaendelea kuitwanga Gaza, wasiwasi wa vita na Iran wazidi

Mchambuzi huyo wa masuala ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini anasema hilo halishangazi kwa sababu tangu kuanza kwa vita vya Gaza, Assad amekuwa akijiweka mbali na mzozo huo wa kikanda huku akijipambanua kuwa mtu asiye na upande wowote. Ana sababu za kufanya hivyo. Kwanza kabisa, kutokana na vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe jeshi lake haliwezi kuwa na vifaa vya kutosha kujibu mashambulizi kwa namna yoyote, pia uchumi wa Syria unadorora na kwa upande mwingine, kutokuwa na upande wowote kwa taifa hilo kwenye mzozo wa Gaza kunaweza kuunufaisha utawala wa Assad katika suala zima la sera za kigeni.

Jeshi la Israel linahofia ongezeko la vikosi vya Iran na miundombinu karibu na mpaka wao

Utawala wa Syria umeonesha mtazamo huo licha ya kwamba Israel imekuwa ikiyashambulia maeneo ya Syria kwa zaidi ya muongo mmoja. Mwaka 2012 Iran ilihusika katika vita vya Syria kwa kuisaidia kupambana na makundi hasimu. Nchi hiyo imekuwa yenye manufaa kwa Iran kwa kutoa njia ya ardhini ya kupitisha silaha na wapiganaji kuelekea Lebanon. Kundi la Hezbollah ambalo ni moja ya mawakala wa kijeshi wenye nguvu ambao Iran inawaunga mkono liko Lebanon pamoja na Syria. Iran na Hezbolla kwa pamoja wanaitambua Israel kuwa adui yao.

Israel yaapa kujibu iwapo Iran itashambulia

Jeshi la Israel limekuwa na wasiwasi na kuendelea kuwepo kwa Iran nchini humo. Linahofia juu ya ongezeko la vikosi vya Iran na miundombinu karibu na mpaka wao, na hii ndiyo sababu Israel imekuwa ikiilenga miundombinu ya Syria mara kwa mara.
Hivi karibuni waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant, álizungumzia mipango ya kutanua kampeni dhidi ya kikosi cha kijeshi cha kundi la Hezbollah chenye makao yake Lebanon. Aliongeza kuwa watafikia  hadi mahali kundi hilo linapoendesha shughuli zao huko Beirut, Damascus na maeneo mengine ya mbali.

Je, mvutano kati ya Iran na Israel unaweza kuwa vita kamili?


Tamko hilo lilifuatiwa na shambulio linalodaiwa kufanywa na Israel katika ubalozi mdogo wa Iran, ambapo watu saba waliuwawa wakiwemo makamanda wa ngazi ya juu wa Iran na wanachama wa Hezbollah.
Hofu ya mashambulizi zaidi ya moja kwa moja ya Israel na Iran inaonekana kutulia kwa sasa. Hata hivyo wachambuzi wanakubaliana kuwa mashambulizi yasiyo ya moja kwa moja huenda yakatokea.