BEIRUT: Jeshi la Lebanon lawashambulia wanamgambo wa Fatah al Islam | Habari za Ulimwengu | DW | 30.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT: Jeshi la Lebanon lawashambulia wanamgambo wa Fatah al Islam

Jeshi la Lebanon limesema linaendelea na mashambulio dhidi ya maficho ya wanamgambo wa kundi la Fatah al Islam ndani ya kambi ya wakimbizi ya Nahr el Bared.

Wanamgambo hao wamekwama ndani ya kambi hiyo kaskazini mwa Lebanon kwa zaidi ya miezi miwili.

Mwanajeshi mmoja wa Lebanon aliuwawa kwenye mapambano ya jana.

Jeshi la Lebanon limesema mara kwa mara linaahirisha uvamizi wa mwisho dhidi ya wanamgambo likihofia usalama wa raia waliosalia ndani ya kambi hiyo.

Zaidi ya wakaazi 30,000 wamehamishwa kutoka kambi hiyo, lakini inadhaniwa wake na watoto wa wanamgambo wa kundi la Fatah al Islam, bado wamo ndani ya kambi hiyo.

Zaidi ya watu 200 wameuwawa tangu mapigano kati ya wanajeshi wa Lebanon na wanamgambo wa kundi hilo yalipoanza kwenye kambi ya Nahr el Bared.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com