1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Bashar al-Assad

Bashar Hafez al-Assad ndiye rais wa Syria, Amiri jeshi mkuu wa vikosi vya jeshi la Syria, Katibu mkuu wa chama tawala cha Ba’ath na Katibu wa Kanda wa tawi la chama hicho nchini Syria.

Julai 10, 2000 Assad alichaguliwa kuwa rais, akimrithi baba yake Hafez Assad, alieiongoza Syria kwa miaka 30 na alifariki mwezi moja kabla. Katika chaguzi za mwaka 2000 na 2007, Bashar alipata kura zaidi ya asilimia 90, katika uchaguzi usiyokuwa na ushindani ambako wagombea wengine hawakurusiwa kupambana naye. Julai 16 2014, Bashar aliapishwa kwa muhula mwingine wa miaka 7, baada ya ushindi katika uchaguzi wa Juni uliyoghubikwa na utata, ambapo aligombea dhidi ya wapizani wawili walioruhusia na serikali, uchaguzi wa kwanza kushindaniwa katika historia ya chama cha Ba’ath cha Syria.

Onesha makala zaidi