1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Abdel-Fattah el Sisi

Abdel-Fattah Saeed Khalil Hussein el Sisi, almaarufu Sisi ndiye rais wa sita na wa sasa wa Misri, akiwa madarakani tangu Juni 2014.

Akiwa mkuu wa majeshi ya Misri, Sisi alimpindua rais Mohammad Mursi kufutaia maandamano ya umma kupinga uongozi wake, na baada ya hapo alianzisha ukandamizaji wa kikatili dhidi ya wafuasi wa Mursi, ambamo watu 1,400 waliuawa na wengine 16,000 kufungwa. Sisi alizaliwa Gamaleya katika mji wa zamani wa Cairo na alihitimu masomo katika chuo cha kijeshi cha Misri. Aliteuliwa na rais Mursi Agosti 12, 2012 kuwa mkuu wa majeshi, waziri wa ulinzi na uzalizaji wa jeshi, akichukuwa nafasi hiyo kutoka kwa Mohamed Hussein Tantawi.