1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Mohammed Mursi

Mohamed Morsi ni mwanasiasa wa Misri na rais wa tano wa taifa hilo kuanzia Juni 30 2012 hadi Julai 3 2013, alipopinduliwa na mkuu wa majeshi Abdel-Fatah al-Sisi, kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake.

Morsi alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia katika historia ya taifa la Misri. Morsi ni msomi aliefikia ngazi ya PhD na alikuwa mwanachama mwandamizi wa kundi la Udugu wa Kiislamu, akichaguliwa kuwa mwenyekiti wa tawi la kisiasa la kundi – Chama cha Haki na Uhuru FJP, kilichoundwa na Udugu wa Kiislamu baada ya mapinduzi ya mwaka 2012, baada ya Morsi na wengine kutoroka gerezani. Mursi aligombea urais na kushinda katika kito hicho katika duru ya pili iliyompabanisha na Ahmed Shafik, waziri mkuu wa mwisho wa rais Hosni Mubarak.

Onesha makala zaidi