1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

RAF

Kundi la Red Army Faction, linalojulikana pia kama Baader-Meinhof au Baader-Meifhof gang lilikuwa kundi la kijeshi la siasa kali za mrengo wa kushoto katika Ujerumani Magharibi. RAF lilianzishwa mwaka 1970.

Viongozi wake muhimu wa kwanza walikuwa pamoja na Andreas Baader, Gudrun Ensslin, Hosrt Mahler na Ulrike Meinhof miongoni mwa wengine. Serikali ya Ujerumani Magharibi ililichukulia kundi la RAFkuwa la kigaidi. Red Army Faction lilihusika katika matukio kadhaa ya urupuaji mabomu, mauaji, utekaji nyara, wizi wa mabenki, na ufyatulianaji risasi na polisi katika kipindi cha miongo mitatu. Shhughuli zao zilifikia kilele mwaka 1977 na kusababisha mgogoro wa kitaifa uliokuja kujulikana kama "Mapukutiko ya Ujerumani".