Zimbabwe yazikosoa nchi za Magharibi | Matukio ya Afrika | DW | 01.12.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Zimbabwe yazikosoa nchi za Magharibi

Zimbabwe imezishutumu nchi za Magharibi kwa kuendeleza ubaguzi kutokana na shinikizo zao za kumtaka Rais Omar El-Bashir wa Sudan akamatwe kwa makosa ya uhalifu wa kivita.

Katika hotuba yake ya hapo jana huko Libya katika mkutano baina ya Umoja wa Ulaya na Afrika Rais Robert Mugabe amesema  anashangaa  ni kwa nini Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya ICC haijawashtaki aliyekuwa waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, na aliyekuwa rais wa Marekani. George W. Bush, kwa ukatili waliotekeleza nchini Iraq ambapo maelfu ya Wairaqi waliuawa.

Serikali ya Sudan ilisema imesusia vikao vya kongamano hilo kama hatua ya kupinga uamuzi wa Umoja wa Ulaya kwamba Bashir asihudhurie vikao vya kongamano hilo.

Wakati huo huo rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel Barosso, akizungumza kwenye mkutano huo wa kilele amesema Afrika inayo nafasi nzuri ya kustawi, kiuchumi, iwapo itashirikiana kikamilifu na Bara la Ulaya.

Ulaya imeahidi kuongeza kiwango cha msaada kwa mataifa ya Afrika hadi Euro bilioni 50 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.  Kwa wakati huu, China inadhibiti soko la Afrika kwa asilimia 2.6, huku bara zima la Ulaya likiwa na asilimia 6 pekee ya soko la Afrika.

 • Tarehe 01.12.2010
 • Mwandishi Yusuf Ramadhani Saumu
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/QN2J
 • Tarehe 01.12.2010
 • Mwandishi Yusuf Ramadhani Saumu
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/QN2J
Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com