1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Morgan Tsvangirai

Morgan Richard Tsvangirai ni mwanasiasa wa zimbawe aliewahi kuwa waziri mkuu kunazia 2009 hadi 2013. Ndiye Rais wa chama cha Movement for Democratic Change - Tsvangirai na ni mpinzani muhimu dhidi ya Rais Robert Mugabe.

Tsvangirai ndiye alikuwa mgombea wa MDC katika uchaguzi wa rais wenye utata wa mwaka 2002, akishindwa na Rais Mugabe. Baadae aligombea duru ya kwanza ya uchaguzi wa 2008, kama mgombea wa chama cha MDC-T, na kupata asilimia 47.8 ya kura kwa mujibu wa matokeo rasmi, na kumuweka mbele ya Mugabe aliepata asilimia 43.2. Tsvangirai alidai kushinda wingi wa kura na kwamba kura hizo zilibadilishwa katika mwezi wa kati ya uchaguzi na kutangaza matokeo rasmi. Awali alipanga kushiriki katika duru ya pili, lakini alibadili uamuzi kabla ya kufanyika, akielezea wasiwasi kwamba usingekuwa huru na wa haki kutokana na kuenea kwa matukio ya vitisho na ukandamizaji vilivyofanywa na wafuasi wa serikali, ambavyo vilisababisha watu 200 kuuawa.

Onesha makala zaidi