Kifo cha Morgan Tsvangirai ni mshtuko na huzuni | Matukio ya Afrika | DW | 15.02.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Zimbabwe

Kifo cha Morgan Tsvangirai ni mshtuko na huzuni

Serikali ya Zimbabwe imesema iko tayari kusaidia katika gharama za mipango ya mazishi ya Morgan Tsvangirai kama hatua mojawapo ya kumuenzi kiongozi huyo wa upinzani ambaye amefariki baada ya kuuguwa kwa muda mrefu.

Kiongozi maarufu wa upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia. Tsvangirai aliyekuwa kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC) alifariki jana Jumatano baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na maradhi ya saratani ya utumbo. Alifariki akiwa na umri wa miaka 65 huko nchini Afrika Kusini alikokuwa anatibiwa.

Marehemu Morgan Tsvangirai aliyekuwa kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe (Getty Images/AFP/Z. Auntony)

Marehemu Morgan Tsvangirai aliyekuwa kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe

Kifo cha Morgan Tvangirai kimepokelewa kwa mshtuko na huzuni kubwa. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na serikali ya Botswana wametoa rambirambi zao. Naibu katibu mkuu wa chama cha ANC nchini Afrika Kusini Jesse Duarte amesema chama chake kimepokea habari za kifo cha kiongozi huyo wa chama cha MDC bwana Morgan Tsvangirai kwa huzuni kubwa.

Bi Duarte amesema chama cha ANC kinatoa rambirambi zake kwa familia ya Bw Tsvangirai na wafuasi wote wa chama cha MDC. Wazimbawe wamesema kifo cha kiongozi huyo wa upinzani ni hasara kubwa kwa taifa kma anavyoeleza bwana Robson Musarafu.

Wafuasi wa chama cha upinzani cha MDC nchini Zimbabwe (Getty Images/AFP/J. Njikizana)

Wafuasi wa chama cha upinzani cha MDC nchini Zimbabwe

Mwanasiasa huyo maarufu zaidi wa Zimbabwe na aliyekuwa kiongozi wa vyama vya wafanyakazi katika sekta ya migodi Morgan Tsvangirai amekimekiwacha chama chake cha MDC ndani ya hali isiyoeleweka miezi mitatu baada ya jeshi nchini Zimbabwe kumng'oa madarakani kiongozi wa muda mrefu, Robert Mugabe, huku uchaguzi nchini Zimbabwe ukiwa unafanyika ndani ya miezi sita ijayo.

Mwandishi: Zainab Aziz/RTRE/AFPE

Mhariri: Josephat Charo