1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Movement for Democratic Change - Tsvangirai

Movement for Democratic Change - kinachofahamika zaidi kama Movement for Democratic Change Zimbabwe - Tsvangirai, ni chama cha kisiasa, na kwa sasa ndiyo chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe.

Chama hicho kiliundwa kutokana na kuvunjika kwa chama cha awali cha Movement for Democratic Change mwaka 2005. Chama cha MDC kiliundwa mwaka 1999 kama chama cha upinzani kwa ZANU-PF chake Rais Robert Mugabe. Chama hicho kiligawanyika baada ya uchaguzi wa seneti wa mwaka 2005, ambapo kundi kuu liliongozwa na kiongozi mwasisi Morgan Tsvangirai na kingine kiliongozwa na Arthur Mutambara. Hatimaye vyama hivyo viwili vilishinda wingi wa pamoja wa viti katika uchaguzi wa bunge wa Machi 2008.

Onesha makala zaidi