Ziara ya Mkuu wa Kanisa la Othodox la Ugiriki Papa Theodorus II | Masuala ya Jamii | DW | 02.03.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Ziara ya Mkuu wa Kanisa la Othodox la Ugiriki Papa Theodorus II

Inaelezewa kuwa imekuwa ya kufana

Ziara ya Mkuu wa Kanisa la Othodox la Ugiriki Papa Theodorus wa pili iliyoanza tarehe 20 mwezi huu Tanzania yenye lengo la kusaidia sekta za elimu na Afya imeelezewa kuwa ya mafanikio.

Bila shaka moja wapo ya mafanikio hayo ni kuzingatia ukweli kuwa mkuu huyo alikuja Tanzania akiwa amepakata kitita cha shilingi bilioni nne za kitanzania ambazo zimelenga kusaidia katika sekta za elimu na afya. Lakini sehemu kubwa ya fedha hizi zinaelekezwa katika kuendeleza shule 6 na Hospitali nne. Sehemu nyingine ya fedha hizo inametolewa katika vituo vya kulelea watoto yatima.

Wachambuzi wa mambo hasa wenye mtizamo wa kidini wanaliona fanikio lingine kuwa ni la baraka za kiroho. Kila mara akiwa nchini au anapokutana na makundi mbalimbali Papa Thodorus wa II hakuacha kutoa mibaraka yake, kwa waumini, wananchi na kwa Tanzania kama nchi.

Mojawapo ya mibaraka iliyotolewa na mkuu huyu ni pamoja na ”Mti huu utakua na wakati ule ule kuleta amani na upendo katika Tanzania na Afarika nzima, na maji ya mvua yataunyeshea kutoka mbinguni kama vile baraka za MUNGU zitakavyokuwa zikiinyeshea Tanzania”.

Alitoa mbaraka huu wakati akiumiminia mti maji ya kutoka mto nile baada ya kuupanda katika kituo cha kulelea watoto yatima jijini Dar es salaam.

Papa Theodorus wa pili aliwasili Tanzania mnamo tarehe 20 mwezi uliopita na amekuwa akiitembelea miradi mbalimbali hasa inayoendeshwa na kufadhiliwa na Kanisa lake.

Mkuu huyu wa Kanisa hili ambaye kwa asili ni Mmisri na makao yake makuu yapo Alexandria anaongozana na balozi wa Misri nchini Tanzania Bwana Sabri Sabry.

Balozi huyo anaitizama ziara ya Mkuu huyo wa Kanisa la Kiothodox, kuwa yenye mafanikio makubwa.

” Ndio ziara ya mkuu hii ni zaiara yake ya kwanza kwa Tanzania akiwa kama Papa na kama mkuu wa Kansia la Kiothodox la Alexandria na katika Afrika nzima hii ni zaiara yake ya kwanza.

Alianza na Afrika Kusini, ambako alitembele Makanisa mengi na miradi mingi kule na akakutana na kiongozi wetu mkuu Nelson Mandela na baada ya hapo akatembelea Zimbabwe na huko miradi mingi pia na rais Mugabe pia na kisha sasa hii ni zaira aliyoianza tarehe 20, ataendelea na ziara yake hadi tarehe 3 mwezi wa march”, anasisitiza Bwana Sabary.

Mojawapo ya vituo vya kulelea watoto yatima alivyotembelea mkuu huyu ni pamoja na kituo kinachyoendeshwa na shirika la Kimataifa la kulea watoto yatima la SOS.

Sehemu ya kujenga kituo hiki ilitolewa na serikali ya Tanzania bila malipo ya aina yoyote. Waziri wa Sheria wa Tanzania Bi Mary Nagu alikuwepo katika kituo hiki na kuwaambia waandishi wa habari, kuwa serikali inafanya kila linalowezekana kuhakikisha watoto yatima wanaendelezwa.

” hata Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Kikwete nyinyi wenyewe mmekuwa mashahidi kuwa amekuwa akifanya mambo kwa ajiri ya kuwasaidia watoto hawa”.

Kwa upande wake Papa Theodorus wa II anaishukuru sana serikali ya Misri kuwa imekuwa ikimsaidia kwa hali na mali katika kufanikisha kazi zake za Kanisa na hata ziara zake.

Lakini pia anakwenda umbali wa kumshukuru mke wa rais wa Misri Binafsi Bi. Suzana Mubaraka kuwa amefanya mengi kwa ajiri ya kuwasaidia watoto yatima na wenye shida nchini Misri.

”tunapofanya majaribio hapa Tanzania Suzana Mubaraka Mke wa rais wa Misri amejitahidi kufanya mengi kwa ajiri ya watoto yatima katika nchi ya Misri, amefanya mengi kwa ajiri ya kuwasaidia watoto wa misri na hiyo ni kitu muhimu sana kwa ajiri ya watoto yatima”.

Kituo kikubwa cha kulelea watoto yatima ambacho kimejengwa karibu na Chuo kikuu cha Dar es salaam kina lengo la kulea watoto yatima zaidi ya 100 kwa wakati mmoja kwa mtindo wa familia.

Kituo hiki kimejengwa kwa ufadhili wa shirika la Kimataifa la kulea watoto yatima la SOS. Papa Theodorus wa II analisifu sana shirika hili kuwa limefanya kazi nzuri sehemu mbalimbali ulimwenguni. Mojawapo ya sehemu hizo ni pamoja na maeneo ya Sethalonike na Athen nchini Ugiriki.

Binafsi anasema hivi sasa Kanisa lake la Othodox la Ugiriki lina wajibu mkubwa kwani ” linatoa misaada ya kimaendeleo katika nchi 53 ulimwenguni” na tanzania ikiwa moja ya nchi hizo.

Mwisho.

 • Tarehe 02.03.2007
 • Mwandishi Christopher Buke
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHlX
 • Tarehe 02.03.2007
 • Mwandishi Christopher Buke
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHlX

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com