1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zambia yatwaa kombe la challenge

Aboubakary Liongo11 Desemba 2006

Nchini Ethiopoea hapo Jumapili timu ya Zambia ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa challenge kwa nchi za afrika mashariki na kati, baada ya kuifunga Sudan penalti 11-10.

https://p.dw.com/p/CHcs
Hali kadhalika: Zidane aenda kwao Algeria
Hali kadhalika: Zidane aenda kwao AlgeriaPicha: AP

Ilibidi mbabe apatikane kwa changamoto ya mikwaju ya penalti, baada ya timu hizo kuwa suluhu hata pale mpambano uliporefushwa.

Zambia ambayo iliingia katika michuano hiyo kama timu alikwa pamoja na Malawi, imechukua kitita cha dola 30,000, lakini si kikombe kilichukuliwa na Sudan kwani Zambia si mwanachama wa CECAFA.

Mlinda mlango Zambia George Kolala alikuwa shujaa baada ya kuokoa penalti mbili.

Mapema Rwanda ilifanikiwa kuchukua nafasi ya tatu baada ya kuifunga Uganda mabao 4-2, katika mchezo ambao pia uliamuliwa kwa mikwaju ya penalti, baada ya timu hizo kutoka suluhu bin suluhu.

Rwanda imechukua kitta cha dola 10,000.Nchi jirani Burundi iliondoshwa katika robofainali, hatua ambayo imewasononesha washabiki wa huko.

Turejee hapa barani Ulaya, ambapo katika ligi kuu ya Uingereza, Chelsea ilitoka sare ya bao 1-1 na Arsenal na hivyo kupanua mwanya kati yake na vinara wa ligi hiyo Manchester United kwa pointi 8.

Hata hivyo kocha wa Chelsea, Jose Morinho amemuonya kocha wa Manchester United Sir Alex Furgeson kuwa asidhani mbio za kuwania ubingwa zimefikia mwisho.

Mourinho amesema kuwa anajua Mzee Furgeson atakuwa na raha kuona Chelsea wametoka sare, lakini asidhani mambo yamekwisha, akifikiria hivyo atakuwa anajidangaya.

Hapa ujerumani katika ligi ya daraja la pili ambayo ni ngumu, Hansa Rostock inazidi kuongoza ikiwa na pointi 36, pamoja na kwamba mwishoni mwa wiki ililazimishwa kutoka sare ya bao 1-1 na TSV 1860 Munich

Nchini Hungary nchi hiyo hapo siku ya jumamosi ilikuwa siku ya maombolezo wakati wa mazishi ya shujaa wa soka nchini humo Ferenc Puskas, aliyefariki tarehe 17 nov akiwa na umri wa miaka 79.

Pusca alikuwa chahu kubwa kwa timu ya Humngary iliyoshinda medali ya dhahabu katika michuano ya Olympic mwaka 1952.

Huko mjini Tokyo kuna michuano ya klabu bingwa ya dunia, ambapo hapo siku ya jumapili mabingwa wa afrika Ahly walifanikiwa kuingia nusufainali baada ya kuifunga Aucland City ya Ocenia mabao 2-0.

Mabao ya Ahly yaliwekwa wavuni na muangola Flavio na mchezaji bora wa afrika Mohamed Aboutrika.Ahly watapambana na mabingwa wa marekani kusini, Internacional ya Brazil.

Nusufainali nyingine itakuwa ni kati ya mabingwa Ulaya Barcelona na mshindi kati ya Club America ya Mexico na Chonbuk Motors ya Korea Kusini.

Barcelona inapigiwa upatu kutwaa uchampion huo na ilipowasilia jana mjini Toyo ililakiwa na washabiki wa kijapan zaidi ya 200.

Michuano hiyo inashirikisha mabingwa wa Ulaya,America Kusini,America ya kati na Kaskazini, Afrika, Asia na Ocenia.Michuano hiyo imechukua nafasi ya ile ya zamani ambapo ilikuwa ni mpambano kati bingwa wa Ulaya na America kusini, toka mwaka 1960.

Tuelekee tana huko barani afrika, ambapo mwanasoka gwiji duniani Zinedine Zidane yuko nyumbani kwaoa likozaliwa Algeria, kwenda kukagua miradi ya hisani alofungua huko.

Zizou akifuatana na mama na baba yake alitabasamu wakati aliposhuka uwanja wa ndege wa Algers, lakini hakusema kitu,kwa waandishi na wapiga picha kiasi cha 150 uwanjani hapo.

Alipokelewa na waziri wa vijana, pamoja na waziri wa kazi wa nchi hiyo, ambapo aliondoka katika benz nyeusi na kuelekea katika kijiji kilichoko kilomita 80, mashariki mwa algears ambako anafadhili mradi nafuu katika eneo hilo lililokubwa na tetemeko kubwa la ardhi mwaka 2003.

Kiasi cha watu 2,300 walikufa , zaidi ya 10,000 wakijeruhiwa huku zaidi ya 100,000 wakiachwa bila ya makazi.

Zizou ambaye anachukuliwa kama mwanasoka bora kabisa katika kizazi hiki alitundika madaluga, kwa timu yake ya taifa baada ya mechi ya fainali ya dunia hapa ujerumani iliyomshuhudia akimtwanga kichwa materazi wa Italia baada ya kumtusi.

Aghlabu sana amekuwa akitembelea Algeria nchi ambayo alizaliwa kabla ya kuhamia ufaransa yeye na wazazi wake wakati huo akiwa mtoto.