1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON:Wafungwa 46 waachiwa kabla mjumbe wa UN kuwasili

2 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ab

Uongozi nchini Myanmar umewaachia huru watu 46 waliokuwa wanazuiliwa tangu maandamano ya kudai demokrasia kufanyika mwezi Agosti na Septemba.Wengi ya wafungwa hao ni wanachama wa National League for Democracy NLD.Hatua hii inachukuliwa ikiwa ni siku moja kabla kuwasili kwa Ibrahim Gambari mjumbe wa umoja wa mataifa.

Hii ni ziara ya pili ya mjumbe huyo maalum na anatarajiwa kushinikiza viongozi wa kijeshi wa Myanmar kufanya mabadiliko ikiwemo hatua ya kuwaachia huru mamia ya watu wanaoaminika kuzuiliwa tangu maandamano ya kudai demokrasia kuanza.

Yapata watu 165 waliokamatwa katika maandamano hayo wameachiwa katika juma lililopita lakini wengi ya wanachama wa upinzani wa NLD bado wanazuliwa.Takriban watu 13 walipoteza maisha yao na wengine alfu 3 kuzuiliwa wakati uongozi wa kijeshi ulipowavamia waandamanaji hao.