1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Mpira wa Miguu

Mpira wa miguu wa vyama - maarufu zaidi kama kandanda au soka, ni mchezo wa timu unaochezwa kwa kutumia mpira wa duara kati ya timu mbili za wachezaji 11 kila mmoja. Mchezo huo unachezwa na wachezaji milioni 250 duniani.

Soka ndiyo mchezo unaopendwa zaidi duniani, na unachezwa kwa kufuata kanuni kadhaa maarufu kama sheria za mchezo. Mchezo wa soka unasimamiwa kimataifa na shirikisho la mpira wa miguu duniani, FIFA, linaloandaa kombe la dunia kwa wanaume na wanawake kilabaada ya miaka minne. Kombe la dunia la FIFA limefanyika kila baada ya miaka minne tangu mwaka 1930, ukiacha mashindano ya 1942, na 1946, yaliofutwa kwa sababu ya vita vikuu vya dunia. Ukurasa huu ni mkusanyiko wa maudhui za DW kuhusu mpira wa miguu.

Onesha makala zaidi