Katibu Mkuu wa CAF Veron Mossengo ajiuzulu
29 Machi 2026
Matangazo
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF, Veron Mossengo-Omba, amejiuzulu wadhifa wake huo Jumapili (Machi 29,2026).
Uamuzi huu unakuja wakati CAF inakabiliwa na ukosoaji mkubwa baada ya kuondolewa taji la Kombe la Afrika kutoka Senegal na madai ya ufisadi ndani chombo hicho cha kandanda barani Afrika.
Mossengo-Omba, mwenye umri wa miaka 66, amesema anaacha kazi ili kujihusisha na miradi yake binafsi, lakini anatarajiwa kugombea urais wa shirikisho la soka la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, FECOFA. Hatua hii inafuatia changamoto kubwa kwa uongozi wa CAF na mashaka kuhusu uadilifu wa mashindano ya soka barani Afrika.