1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Soka: Klabu zilizotinga 16 bora ya Champions League

26 Februari 2026

Hatimaye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya maarufu UEFA Champions League imefikia katika hatua ya 16 bora.

https://p.dw.com/p/59SGN
Champions League 2026 | Inter Mailand vs. Bodø/Glimt | Wachezaji wa Bodø/Glimt wakifurahia ushindi unaowapeleka hatua ya 16 bora:
Wachezaji wa Bodø/Glimt wakifurahia ushindi dhidi ya Inter Milan Picha: Piero Cruciatti/AFP

Siku ya Jumanne na Jumatano zilishuhudiwa mechi za mchujo kwa timu ambazo hazikufanikiwa kufuzu moja kwa moja katika hatua hiyo ya ligi ya mabingwa.

Mabingwa wa mara nyingi wa michuano hiyo Real Madrid waliendeleza ubabe wao kwa Benfica ya Ureno kwa kuwacharaza 2-1 katika mechi ya marudiano na kusonga mbele hatua ya 16 bora.

Mechi ya awali iliyokubwa na misukosuko kwa tukio la nyota wa Real Madrid, Vinicius Jr kudai kufanyiwa vitendo vya ubaguzi na mchezaji wa Benfica, Madrid alishinda 1-0.

PSG ya Ufaransa ambayo ndiyo mabingwa watetezi nayo ilifanikiwa kufuzu japo kwa mbinde baada ya sare ya 2-2 dhidi ya majirani zao Monaco. Sare hiyo imeifanya PSG kusonga mbele kwa jumla ya magholi 5-4.

UEFA Champions League 2026 | Mechi ya mchujo kati ya SL Benfica na Real Madrid | Prestianni na Vinicius wakipambana
Mechi ya mchujo kati ya SL Benfica na Real Madrid | Prestianni na Vinicius wakipambanaPicha: Irina R. Hipolito/ZUMA/IMAGO

Borussia Dortmund ya Ujerumani imetupwa nje ya michuano hiyo baada ya kuambulia kichapo cha magoli 4-1 dhidi ya Atalanta ya Italia.

BVB walishinda mchezo wa kwanza 2-0 mjini Dortmund dhidi ya waitaliano hao lakini waliposafiri kwenda Italia waliangua pua.

Droo ya Robo fainali kufanyika Ijumaa

Jumla ya timu 16 zinaisubiria kwa hamu droo ya mechi zao zijazo itakayofanyika Ijumaa nchini Uswisi.

Timu hizo ni Arsenal, Bayern München, Liverpool,Tottenham, Barcelona, Chelsea, Sporting CP, Man City, Real Madrid, PSG, Newcastle, Atletitico Madrid, Atalanta, Leverkusen, Galatasaray, na Bodø/Glimt.

Fainali ya UEFA msimu huu itachezwa mjini Budapest, Hungary tarehe 30, Mei.