1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Ukuta wa Berlin

Ukuta wa Berlin ulijengwa na serikali ya Ujerumani Mashariki 1961.Ukuta huu ukiutenganisha upande wa Magharibi wa mji wa Berlin mbali na upande wa Mashariki, pamoja na eneo zima la Ujerumani mashariki.

Upande wa Mashariki unadai kwamba ukuta ulijengwa ili kulinda siasa zao za kisoshalisti za iliyokuwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani, GDR. Na upande wa Magharibi, unadai kuwa ulijengwa ili kuzuia mmiminiko wa wahamiaji wakati wa vita baridi barani Ulaya. Novemba 9, 1989, ambayo ni siku ya kilele cha maandamano ya kupinga uongozi wa GDR, ukuta huwo ulibomolewa. Kuangushwa kwa ukuta huwo, kuliiwezesha Ujerumani kuungana tena rasmi Oktoba 3, 1990. Miaka ishirini na tano baadae, mabaki ya ukuta wa Berlin bado yapo kama kumbukumbu ya yaliyotokea.

Onesha makala zaidi